TANZANIA: Kazi zipo nyingi zinakuja, sema siwezi kuahidi ni lini - Billnas

 

 

 

Msanii wa muziki wa hop hop Billnass amedai amechoka kutoa ahidi zisizo kamilika kwa mashabiki wake kuhusu ujio wake mpya baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Chafu Pozi’.

Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Billnass amesema kwa sasa atakaa kimya mpaka kazi ambazo amepanga kuzitoa zikamilike.

“Kazi zipo na zinakuja sema siwezi kuhaidi ni lini kwa sababu tayari ameshaahidi sana,” alisema Billnass. “Kuna mambo hayaendi sawa, sisi tunapanga yetu na Mungu anapanga yake. Kwahiyo mashabiki wakae tu mkao wa kula kuna mambo mazuri yanakuja hivi karibuni,”. Rapa huyo ni mmoja kati ya wasanii vijana waliofanya vizuri ndani ya mwaka 2016.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment