Lyrics
Baada ya kumaliza primary la saba Mamu mjini Dar
Akapata mchumba, mji wa Mwanza Mamu akampendaa
Kwa kuwa Mamu alimpenda sana hivyo akaona vyema nyumbani kusema
Akamuambia mama, kwamba mama nimeshapata mchumba
Mama akagombaa, akagomba huku akisemaa life has changed eeeeh
View moreMwanangu somaa (eeeh aeeh) life has changed (eeeh)
Achana na mabwana (eeeh aeeeh) life has changed (eeeh)
Mwanangu somaa (eeeh aeeh) life has changed
Kusema kweli sikuamini, nilivyomkuta Mwanza mjini Mariamu aaaaiih
Kusema kweli sikuamini, nilivyomkuta Mwanza mjini Mariamu aaaah
Aibu kwani amekwisha kabisa, hata umbo lake zuri la mvuto lishapoteaaa
Ni kweli amekwisha kabisa, hata umbo lake zuri la mvuto lishapoteaaa
Mamu wa Daar
Baada ya wazazi wake kugomba juu ya swala lake Mamu la kuolewa
Ikabidi atoroshewe jijini Mwanza na mchumba kwake
Maisha yao Mwanza yalikuwa mazuri,
Yalikuwa mazuri tena ya kitajili,
Ndipo akazaa na watoto, mwanzo wa mateso huo kwa Mamu
Mume wiki hayupo home na anaporudi home Mamu atuliza kipigo!
Nifanye nini swali ambalo alikuwa nalo
Au nirudi kwa mama home?
Ila nitamuelezaje ili anipokee? Mamu aliwaza bila kupata jibu
Mara mume anarudi, kichwani mitungi,
Kaanza kumdunda Mamu mwisho akamtimua
Huruma, kwani ana watoto watatu na anatanga na njiaa
Huruma pale anapoulizwa na watu akiwasimuliaa aah
Kusema kweli sikuamini, nilivyomkuta Mwanza mjini Mariamu aaaaiih
Kusema kweli sikuamini, nilivyomkuta Mwanza mjini Mariamu aaaah
Aibu kwani amekwisha kabisa, hata umbo lake zuri la mvuto lishapoteaaa
Ni kweli amekwisha kabisa, hata umbo lake zuri la mvuto lishapoteaaa
Mamu wa Daa
Sauti ikaskikaa ikisema 'mimi hapa nitakupa room'
Mara mweingine akamshika bega akasema 'kaza moyo nitakupa mtaji'
Mamu alipiga magoti chini na kumshukuru Muumba aaaaah
Mamu alipewa room na mtaji wa kuuza karanga
Akayaanza maisha yake, akilea watoto wake,
Siku moja nikiwa safari, nipo ndani ya gari Mwanza i mean sikuamini
Nilipomuona binti kama Mamu
Lakini vipi Mamu mrembo vile auze karanga?
Nikashuka nikasogeaa niende kumuangalia mara ghafla alianza kuliaa
Akatupa sinia la karanga, kapiga yowe Nasso akanikimbiliaaa (Nasssooo)
Ni wewe Mamu ulosoma na mimi (Nassooo), haya nieleza umepatwa na nini?
Wazazi wako huzuni moyoni, hata bibi yako hayupo duniani
Mamu hivi ndo alivyosema, ninakumbuka ya mama, oooh "Life has changed" eeeh
Ni bora ningesomaa, oooh life has changed eeeh
Aloyasema mama, oooh life has changed eeeh
Ni bora ningesomaa eeeh