TANZANIA: Mrisho Mpoto ampongeza Diamond

 

 

 

Moja kati ya wasanii wenye heshima kubwa nchini na mtunzi wa mashairi na nyimbo zenye mahadhi ya kiafrika, Mrisho Mpoto, kupitia mtandao wa Instagram amemsifia Diamond Platnumz kwa wimbo wake mpya wa 'Salome' na kusema kuwa amemfurahisha sana kwani amefanya wimbo wenye asili ya kwetu Tanzania na hiyo ni heshima kwa nchi.

Kupitia  mtandao wa kijamii wa Instagram, Mpoto ameandika:

“Nassibu kiukweli nimefurahishwa sana na kazi yako ya#Salome imeonyesha ukomavu Mkubwa na team work, kikubwa ukiwa unafanya kazi zenye test ya nyumbani unatupa heshima kama nchi na inakuonyesha wewe ni nani? na nani siyo wewe? Nassibu Mwenda kwao siku zote haogopi Giza, nenda lakini waambie nna kwetu, kama ulivyofanya kwenye Salome. Sisi ni wabantu bwana tunaruhusiwa zaidi ya mmoja, na Mimi ntamtafuta Salome wangu wa ukubwani ashike magoti nisimame kama ngongoti japo nna kitambi ntainama kidogo!!@diamondplatnumz @babutale“

 

 

Unaweza kuitazama Video hiyo ya Salome hapa:

 

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment