TANZANIA: Snura ajiita ‘Malkia wa Uswazi’

 

 

Mwanamuziki na muigizaji nchini, Snura Mushi, ameamua kujipa cheo cha Malkia wa Uswazi pasipo kujali ya kuwa yupo mwanamuziki mwenzake, Shaa, ambaye kuanzia hapo awali alikuwa akijiita kwa jina hilo.

Enewz ilimtafuta Snura na kupiga naye story kuhusu kujiita 'Malikia wa Uswazi' suala ambalo Snura alisema yeye amekulia kwenye maisha ya Uswahilini (Uswazi) na hata nyimbo ambazo anaziimba zina maudhui ya mazingira ya uswahili hivyo hata akijiita ni sahihi.

“Mimi nimeandika vile nikiamini kuwa mimi ni malkia wa uswazi, kwanza nimekulia huko nimekaa huko na hadi sasa hivi bado nakaa huko na nyimbo zangu pia ni za uswazi so sioni kama kuna shida nikijiita malkia wa uswazi.” Amesema Snura Mushi.

Hata hivyo eNewz bado iliendelea kumuuliza kuwa inakuwaje Shaa akisikia kuhusu yeye kujiita malkia wa uswazi lakini Snura bila uoga alisema mimi najiamini na sijali mtu atachukuliaje kuhusu hilo kwa sababu hata mashabiki nao wananiita malkia wa uswazi mara malkia wa kisingeli so sioni shida na hayo yote ni kutokana na muziki wangu na maisha yangu kiujumla.

 

Shaa

 

“Mimi sijali kwamba mtu atachukuliaje kwa sababu hata mashabiki nao wananiita hivyo tena sasa wameongezea kuwa mimi ndio malkia wa kisingeli pia hayo yote ni kutokana na mziki ninaofanya na mwisho wa siku watu tu wenyewe wanajua tu nani malkia wa Uswazi”

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment

Top stories

More News