TANZANIA: Tattoo sijachora kwa ajili ya Freemason – Ruby

 

 

Hit maker wa 'Na Yule', Ruby ambaye kwa sasa amekuwa gumzo, ameingia kwenye 'kiki' nyingine baada ya kuonekana na tattoo yenye jicho ambalo ikadhaniwa kuwa ni moja ya michoro iliyopo kwenye imani ya Freemason.

Ruby alikanusha kuwa katika imani hiyo na kusema kila kuwa mtu ana jicho na hana maana ya kuwa kwenye imani hiyo ya Freemason bali yeye ni Mkristo na anamuamini Mungu.

“Hakuna binadamu bila macho, na mimi ni mkristo namuamini Mungu so sijawahi kuingia kwenye Freemason so hizo ni imani za watu na hiyo tattoo sijachora kwa ajili ya Freemason.” Amesema Ruby.

Pia kuhusu uongozi Ruby ameweka wazi kuwa kwa sasa anajisimamia yeye mwenyewe, “Nimeamua kubadili uongozi na sasa najisimamia mwenyewe kwa ajili ya mashabiki wangu”.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment