TANZANIA: Ninavyoamini mimi hakuna hip hop singeli ila kuna muziki wa singeli - Stamina

 

 

Rapa Stamina amemtaka Prof Jay atoe maelezo ya kutosha kutokana na jina la “Hip Hop – Singeli” alilolitumia katika ngoma yake mpya aliyotoa na Sholo Mwamba.

Hiyo ni baada ya Mbunge wa Mikumi na mwanamuziki mkongwe wa hip hop nchini, Proffessa Jay kufanya ngoma na Sholo Mwamba wimbo wa 'Kazi Kazi' na kusikika akisema “Hip Hop – Singeli”.

Stamina alifanya mahojiano na eNewz na kusema kuwa anacho fahamu ni kwamba kuna Hip hop ikiwa inajitegemea na Singeli ikiwa na muziki mwingine, na anachojua ni kuwa Professa Jay ameimba kwenye biti ya singeli lakini si kuipa jina la hip hop singeli.

“Mimi najua kwamba Professa Jay kaimba kwenye biti ya kisingeli na sio kwamba kaimba hip hop singeli kwa kuwa kwa ninavyoamini mimi hakuna hip hop singeli ila kuna muziki wa singeli na muziki wa hip hop” amesema Stamina.

Hata hivyo Stamina alisema singeli ni muziki ambao ulikuwepo tangu zamani sema ulikuwa unatumika kwenye sherehe za mitaani na maharusini ila sasa umeboreshwa na kuwa wa kisasa ndyo maana watu wanauongelea ila singeli na hip hop ni aina mbili tofauti za muziki.

Pia Stamina alimalizia kwa kusema Professa Jay kaamua kuipa heshima singeli na huenda alisema hip hop singeli kwa kuwa kaimba kwa staili ya ku'rap katika wimbo huo na Sholo Mwamba kaimba staili ya singeli kwa hiyo akaona iwe hip hop singeli.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment