TANZANIA: Mansu-Li amtaka GK kutojiita mwana hip hop

 

 

 

Mkali wa ku'rap Mansu-Li amemuasa msanii mwenzake King Crazy GK asiendelee kujiita mwana hip hop kwa kuwa ametangaza kufanya mziki wa kuimba kwa sasa.

Mbele ya camera za eNewz, Mansu-Li amesema kuwa hawezi kumkataza GK kufanya muziki wa kuimba kwakuwa kila mtu anafanya kitu ambacho anakipenda na kitamuweka karibu na mashabiki zake ila akimtaka asijiite tena mwana Hip hop.

“Siwezi kumkataza asifanye muziki wa kuimba kwa kuwa kila mtu anafanya kitu ambacho kitamuweka karibu na mashabiki zake ila cha muhimu hapaswi kujiita tena mwana hip hop kwa kuwa ha'rap tena” Alisema Mansul-Li.

Mansu-Li amefafanua zaidi sababu yakumtaka GK kutojiita mwana hip hop nikutokana nakuwa muziki mzuri ni ule unao eleweka, msanii mzuri ni yule anaye tambua muziki anao ufanya pasipo kubabaika na kuwachanganya mashabiki wake.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment