TANZANIA: Belle9 atamba kuja na albam ya kumpiku Michael Jackson na Bob Marley

 

 

 

Msanii Belle 9 ambaye ameamua kuvunja ukimya wa albam katika soko la muziki la bongo, amesema anakusudia kutoa albam yake ambayo itakuwa na utofauti mkubwa.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Belle 9 amesema kwenye albam hiyo ameweka ladha tofauti tofauti, na kwa kutumia ubunifu wa hali ya juu, ambao hata wasanii nguli wa muziki duniani kina Michael Jackson na Bob Marley, hawajawahi kufanya.

"Albam yangu ya Vitamin Music itakuwa ni albam ya tofauti, itakuwa na vitu vingi fantastic, itakuwa na jumbe tofauti tofauti, kutakuwa na mada tofauti tofauti za mapenzi, maisha, hustling na pia 'angle' nyingi ambazo wasanii wengi duniani hawazigusi, kama nilivyosema vitamin music, nadhani hata Michael Jackson, Bob Marley hawajawahi kufikiria katika level hiyo, kwa hiyo itakuwa ni albam ambayo ipo strong sana", alisema Belle 9.

Belle 9 aliendelea kusema kuwa lengo la kutoa albam hiyo lilikuwepo muda mrefu, na ni kitu anachokipenda kukifanya.

"Kwangu mimi albam ni kitu ambacho nakifanya, ni kitu ambacho napenda kufanya kwa sababu mi naishi kwenye muziki, kila siku nakuwa studio, nikipata nafasi narekodi vitu tofauti, na mtu ili apate nafasi ya kunisikiliza lazima apate albam yangu", alisema Bell 9.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment