TANZANIA: Hakuna kitu kinaitwa HipHop Singeli – One the Incredible

 

Msanii mkali wa HIPHOP bongo One The Incredible asema hakuna aina ya muziki unaoitwa HipHop singeli na kama utakuja itakuwa ni baadaye sana.
Akiongea ndani ya eNewz One amesema " hakuna kitu kinachoitwa Hiphop singeli unaweza kuchana kwenye biti ya singeli kama alivyofanya Pro. Jay lakini haimaanishi kwa kufanya hivyo ndiyo iitwe Hiphop singeli"


Kwa sasa One The Incredible yupo studio anaandaa albam yake ya 3, ambapo eNewz ilitaka kujua kama ana mpango wa kufanya muziki wa singeli kwenye albam hiyo baada ya Mh. Profesa Jay kuachia ngoma yake ya Singeli “Kazi Kazi” na kusema kuwa kwa sasa hana mpango huo.
One amesema "Hata ukiona wasanii wa nje wanabadilika basi wanakuwa wameshaweka heshima katika muziki wao wanaouimba ndipo wanabadilika kwa kuwa hata muziki wa 'crunk' ni muziki wa zamani lakini kwa sasa ndiyo unapata umaarufu huku Bongo.

Leave your comment