TANZANIA: Bado natamani kufanya kolabo na msanii wa Tanzania - Chidinma

 

 

 

Chidinma alisema hayo alipokuwa akihojiwa kwa njia ya simu kwenye kipindi cha 'The Cruise' ya East Africa Radio na kusema amefurahi sana kufanya kazi na Joh Makini hivyo anatamani kufanya kazi na msanii mwingine wa bongo fleva kutoka Tanzania.

"Nilikutana na Joh Makini Coke Studio na tuliweza kufanya kazi ya 'Perfect Combo' sikuwahi kuwa na mtu wa kunifundisha kuimba kiswahili lakini Joh Makini alifanya hivyo, kiukweli nilifurahi na muda si mrefu nitaanza kutoa kazi zangu, lakini bado natamani kufanya kazi na msanii mwingine kutoka Tanzania" alisema Chidinma

Mbali na hilo Chidinma alisema muziki wa Nigeria umeweza kufanikiwa na kuwa kama utambulisho wa nyimbo za Afrika kutokana na ukweli kwamba wao wapo na uhalisia wao kwa kila kitu wakifanyacho, hawaigi vitu vingine kutoka kwa watu wa Ulaya, ndiyo maana muziki wao umeweza kuwa na nguvu zaidi.

 

Unaweza kutazama “Perfect Combo” ya Joh Makini ft Chidinma hapa:

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment

Top stories