TANZANIA: Mimi na Bill Nas si wapenzi ila sisi ni watu wa karibu sana – Linah

 

 

 

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Linah Sanga amefunguka na kusema kuwa ukaribu alionao na msanii Bill Nas imefanya wao kushauriana mambo mengi kuhusu muziki na nje ya muziki.

Linah anasema alikuwa anatamani siku moja apate mtu ambaye ni rafiki yake ili awe anamueleza mambo yake kama ambavyo imekuwa sasa kwake yeye na Bill Nas

Linah alisema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kudai kwa sasa yeye na Bill Nas siri yake ndiyo siri ya Bill Nas na siri ya Bill Nas ndiyo siri yake yeye.

"Watu wanatakiwa wajue tu kuwa mimi na Bill Nas si wapenzi ila sisi ni watu wa karibu sana, saizi mimi na Bill Nas ni washikaji sana maana siri yake ndiyo siri yangu, Bill Nas ndiye aliyenishauri nibadilike kwenye muziki na kunipa 'connection' na 'Producer' T Touch, yeye ndiye aliniambia nibadili mfumo mzima wa muziki wangu na ndiyo nikafanya hivyo" alisema Linah

Mbali na hilo msanii Linah Sanga amesema kwa sasa hana tena zile stress alizokuwa nazo awali kwani mtu aliyempata anafanya awe na furaha na amani muda wote, na katika kipindi cha ukimya wake amekitumia vyema kuandaa kazi nyingi zaidi.

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment