TANZANIA: Raymond afunguka baada ya mashabiki kuikataa staili yake mpya ya nywele

 

Msanii kutoa kundi la WCB, Raymond amezua gumzo kwa mashabiki zake baada kuonekana na muonekano mpya. Mashabiki wengi walimshambulia kwakutokupendezwa na staili hiyo mpya ya nywele.

 

 

Kupitia kipindi cha Amplifaya ya Millard Ayo Raymond alifunguka na kuyasema haya, “Unajua watu hawakuelewa sikuweka zile rasta kama ni style yangu mpya hapana niliziweka kwasababu ya kufanya photoshoot kwahiyo niliziweka kwa siku moja sasa jioni nikaambiwa niende kwenye event nikaenda nazo hivyo hivyo’- Raymond

 

‘Nimeona comments nyingi kuhusu rasta lakini naomba watu waelewe kwamba haikuwa style yangu na wala sina mpango wa kufuga rasta nitabaki na style yangu moja tu maana inaonekana jinsi nilivyowakwaza mashabiki wangu’- Raymond

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment

Top stories