TANZANIA: Nilishafanya ‘This Love’ kabla ya Maua Sama – Ben Pol
2 August 2016

Msanii Ben Pol ametoa siri ambayo wengi tulikuwa hatuijui, kuhusu wimbo wa 'This Love' alioufanya na Maua Sama.
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Ben Pol amesema wimbo huo alishaufanya na Fundi Samweli na kukamilika kabisa, kabla hajampa Maua Sama aufanye.
“Ule wimbo mimi nilishaufanya, niliuandika nikaurekodi na Fundi Samweli, baadae tunatumiana muziki, nyimbo mpya na nini na Mwana FA, nikamwamba bwana kuna wimbo huu nimeufanya, by the time Mwana FA alikuwa amemgundua Maua, akanitumia wimbo wa Maua alikuwa ameufanya Moshi, nikamwambia huyu dada wa wapi!? Akaniambia nataka nimsign, nikamwambia msaini hata leo, baadae nikachukua ule wimbo nikamwambia sikiliza huu wimbo mkiupenda Maua aufanye, nilikuwa nishaurekodi, ushafanyiwa mixing, nikampa FA akampa Maua, akaenda kuufanya”, alisema Ben Pol.
Pia Ben Pol ameelezea sababu iliyopelekea na yeye kuimba kwenye wimbo, hata baada ya kuugawa kwa Maua.
“Maua akaniambia Ben nimeupenda huu wimbo lakini nahisi nataka wewe ufanye verse pia, nisiimbe wimbo wote uwe mimi ft wewe, tukaenda tukafanya wimbo ukatoka tukaenda kushoot video”, alisema Ben Pol.
Unaweza kuitazama video ya Wimbo wa This Love hapa:
Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz




Leave your comment