TANZANIA: Chidi akumbuke kuna maisha tuliishi kabla hajaingia WCB – Baghdad

 

 

Raper mbabe wa “mistari konzi” ya kuwachana watu Baghdad amesema hatosita kutoa video aliyomshirikisha Chidi Benz na Nay Wa Mitego kwa kuhofia Babu Tale ataifanyia fitna video hiyo ili ifeli.

Baghdad aliwahi kumdiss Babu Tale katika wimbo wake wa Mtazamo Remix kwa mstari uliosema “Game ishakuwa ya wadau, Tale ana nguvu ya kufanya Media house wakudharau”, msitari uliomkashifu Tale kiasi cha kumfanya adhaniwe kuwa na bifu na Baghdad japokuwa mpaka sasa mara chache walizoonana walipiga stori kwa amani. Baghdad alisema “tulikutana katika vikao vya wasanii akaniambia yeye hajanimaindi”.

Lakini hivi karibuni Baghdad alipotaka kuachia video ya wimbo alioshirikiana na Chidi Benz (ambaye kwa sasa anafanya kazi kwa usimamizi wa Babu Tale na WCB), Chidi alimpiga stop baghdad kwa kumwambia asitoe wimbo huo mpaka Babu Tale akague video hiyo, kitendo ambacho Baghdad hakukubaliana nacho.

Akizungumza na eNEWZ Baghdad alimaliza kwa kusema “Chidi akumbuke kuna maisha tuliishi kabla hajaingia WCB, asiithamini laki moja ambayo amepewa na mtu mwenye milioni kumi na tano bali athamini elfu kumi aliyotumiwa na mtu akiwa na shilingi elfu kumi na tano”

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment