TANZANIA: Naogopa kutoka na watoto wadogo kimapenzi – Dayna

 

 

 

Msanii Dayna Nyange ambaye kwa sasa ameachia wimbo wake mpya akiwa ameshirikiana na Bill Nas amefunguka na kusema kuwa yeye kwenye mahusiano hapendi kutoka na watoto wadogo kwani watoto wadogo kwanza wanakomelea sana lakini wanakuwa na mambo mengi.

Dayna Nyange alisema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kusema kuwa mara nyingi anapenda kuwa na mahusiano na watu wazima ambao wanajitambua na kujielewa, kwani watoto wa dogo wanakuwa wanasumbua sana kutokana na umri wao kuwaruhusu kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja hivyo yeye huwakwepa.

"Unajua mimi nina wivu sana hivyo naogopa kutoka na watoto wadogo kimapenzi, lakini pia watoto wadogo wanakuwa na mambo mengi sana unakuta wewe unahitaji kufanya maisha lakini kumbe mwenzako anawaza kuwa na wewe kwa kukomelea tu, pili wanakuwa na mahusiano na watu wengi, wanawaza starehe sana na dunia yetu ya leo hii maradhi mengi, mimi nawaogopa sana vijana" alisisitiza Dayna Nyange.

Mbali na hilo msanii Dayna Nyange aliongea kwa matani huku akicheka na kusema amekuwa akiwakimbia na kuwakwepa sana vijana wadogo sababu wanakomelea sana (wanakamia sana kwenye mapenzi).

"Unakuta wewe umepanga kufanya maisha unakutana na kijana kumbe yeye bado hayupo tayari na bahati mbaya umepata ujauzito hataki si ndiyo hapo utaanza kulea mtoto peke yako, lakini pia vijana wanakomelea sana" aliongea Dayna Nyange huku akicheka.

Dayna Nyange ameachia wimbo wake mpya alioupa jina la 'Komela' ambao ameshirikiana na Bill Nas.

 

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment