TANZANIA: Maisha ya mtandao wa Instagram yamkimbiza Wema kwa muda
21 July 2016

Maisha ya mtandao wa instargam yanamkimbiza kwa muda malkia wa filamu Wema Sepetu baada ya kuvurugwa na watumiaji wa mtandao huo.
Mwanadada Wema Sepetu hakuweka wazi tatizo ni nini lakini ameandika ujumbe mrefu akilalamikia jinsi watu wa kwenye mtandao huo wanavyomwandama kila kukicha.
Kupitia instagram, Wema ameandika:
Naomba niseme kitu na nieleweke tafadhal, Sijawahi hata siku moja kwenda kwa hata mmoja wenu na kumgongea kuomba hata hela ya chumvi…. My life concerns me…. Na hata siku nikifa nakufa mwenyewe, Majibu kwa Mungu naenda kujibu alone…. Niacheni Jamani…. Nimechoka……! Jus leave me Alone…!!! Kama nakukera na maisha yangu basi usiyafatilie… Sio lazima….. Nisiheme sasa…. Naomba tafadhal kama mapungufu ni ya kwangu mimi na mimi mwenyewe sasa midomo inawatoooooooka as if nimeua mtu…… Niacheni bana….. Mi nafanya kile kinachoridhisha nafsi yangu maana sipendi kujikalfisha sasa nyinyi msofanya na nyie kinachowaridhisha mnasubiria nini…..Please baaaaana…. Spare me…… Mniache……..!!! Kwani nikitajirika mimi au nikiwa maskini wewe unapata faida gani… Jiulize kwanza hilo swali ndo uanze kutoa maneno yako….. Remember U also got ur life to live sooooo stop putting ur Nose into other’s Life….. #MyLifeMyRules…. Nakukera….? Sio lazima…. Sijaomba mtu… Ishini maisha yenu…. Silazimishi mtu na sijawahi lazimisha mtu kunisupport…. Kila mtu anafanya out of free will….!!! Ieleweke hio kwanza… Afu mengine yafate….. Nadhani Insta kwa leo inatosha…. Tuonane week ijayo maybe…..!




Leave your comment