TANZANIA: Sihitaji pole kutoka kwa Mkubwa na Wanawe - Shaa

 

 

Mwimbaji Sarah Kaisi a.k.a Shaa ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake mpya ya 'Sawa' amesema kuwa yeye kuweza kuondoka chini ya usimamizi wa Mkubwa na Wanawe pamoja na Master Jay si suala la kupewa pole bali anastahili kupongezwa.

Kuanzia kushoto ni JR Junior, Dulla Mjukuu, Shaa pamoja na Dj Ommy Crazy wakiwa studio za East Africa Radio.

Shaa akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio alisema kuwa moja ya ndoto yake kubwa kwa muda mrefu ni yeye kuwa na kampuni yake, Label yake pamoja na kuwa na studio yake mwenyewe, hivyo kitendo cha mwaka huu kuanza kwa kuwa na kampuni yake ambayo inamsimamia kazi zake ni jambo la kupongezwa kwani anaona amepiga hatua.

"Nimekuwa nikipokea ujumbe mfupi kutoka kwa watu wengi wakinipa pole, mimi kutoka Mkubwa na Wanawe na Mj Records lakini nataka kuwaambia hili si la kupewa pole bali nastahili pongezi, kwani ilikuwa ndoto yangu siku kuja kuwa na kampuni yangu na kuwa na Label yangu mwenyewe. Hivyo mwaka huu kuanza na SK Music ni hatua ila watu wanatakiwa wajue nimeondoka huko lakini Mkubwa na Wanawe na Mj Record kwangu bado wananipa mwongozo, hivyo hata SK Music ni mtoto wa Mkubwa na Wanawe na Mje Records" alisema Shaa

Mbali na hilo Shaa aliweka wazi mpango wake na kampuni yake na kusema kuwa kuanzia mwakani ndiyo wanaweza kutambulisha wasanii waliopo chini ya Label hiyo, japo kwa sasa msanii aliyopo ni yeye mwenyewe.

 

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

 

Leave your comment

Top stories