TANZANIA: Sikumdhalilisha Jay Dee - Gardner

 

Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, Gadner G Habash amekanusha kumdhalilisha aliyekuwa mke wake Lady Jaydee kupitia video ambayo ilisambaa katika mitandao ya kijamii miezi michache iliyopita.

Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii, Gadner amesema anaheshimu faragha ya muimbaji huyo wa wimbo ‘Ndi Ndi Ndi’ na kamwe hawezi kufanya kitendo kama hicho.

“Kusema kweli sitaki kulizungumzia suala la Lady Jaydee, naheshimu faragha yake,” alisema Gadner. “Ile issue ilikuzwa na mitandao ya kijamii, na mitandao ya kijamii inajua kutengeneza mambo hata yasiyokuwepo,”

Mtangazaji huyo amesema hana tatizo na mwanadada huyo kwa kuwa kila mtu alisha ‘move on’ na anaendelea na mambo yake.

Katika video ambayo ilisambaa mitandaoni, Gadner alisikika akisema “Na sina neno na yule mtoto wa kike. Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi,” kauli ambayo ilichukuliwa vibaya na watu wengi.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment

Other news