TANZANIA: Namkubali sana Mwana Fa – Maua Sama

 

 

Maua Sama amedai kuwa angependa kufanya kazi tena na bosi wake wa zamani, Mwana FA. Muimbaji huyo alianza kujulikana kupitia wimbo ‘So Crazy’ aliomshirikisha rapper huyo. Akiongea na mtangazaji wa Jembe FM, JJ, Maua alisema kuwa FA ni rapper anayemkubali zaidi.

Amewataja Fid Q, Bill Nass, Mr Blue, Weusi kuwa ni rappers wengine ambao angependa kufanya nao kazi na kwamba yeye ni shabiki mkubwa wa hip hop ya Tanzania. Aliongeza kuwa ngoma yake ijayo amemshirikisha rapper Stamina.

 

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment