TANZANIA: Nikki Mbishi awachana mameneja wa bongo

 

 

 

Mkali wa Rap Bongo Nikki Mbishi amewachana wanaojiita mameneja Bongo, kwa kusema hawajui wanachokifanya. Nikki amesema yeye hahitaji Meneja sababu mameneja wa Bongo ni "midananda".

Amesema wanakuwa wakiwatumia tu wasanii na ndo maana wasanii wakifulia na mameneja wanafulia pia, kwa hiyo yeye anasema anatafuta promotion agent ambao watakuwa wanamtangazia kazi zake ili kuweza kupata shavu.

Hata hivyo Nikki amewachana wasanii wa siku hizi ambao wanatumia nguvu sana kujipromoti wakati hawafanyi muziki mzuri na kusema wanatakiwa kufanya muziki mzuri kwani itafikia kipindi hawatahitajika stejini.

Nikki amemalizia kwa kusema wasanii wa sasa wanapanga show ya wasanii hata thelathin na bado hawajazi ukumbi wakati ukimuweka msanii kama Juma Nature anajeza ukumbi yeye mwenyewe na watu wanaenjoy.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment