TANZANIA: Msechu amesema 'soon' atafunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu

 

 

Msanii nguli wa bongo fleva Peter Mshechu hivi karibuni amemvisha mpenzi wake Pete ya uchumba. Mwanadada huyo ameishi naye kwa muda mrefu wa takribani miaka kumi na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike.

Msechu amefunguka ndani ya Enews na kusema mwanadada huyo (Amariss Muffa) amemvumilia kwa mambo mengi na kusema kwamba raha ya mwanadada huyo ni kitambi chake hivyo hajali wadau wa mjini wanao 'mdiss' kuhusiana na unene wake.

Hata hivyo Msechu amesema kuwa 'soon' atafunga ndoa na mwanadada huyo na baada ya ndoa tu watu watarajie watoto wengi kutoka kwao kwani ni kitu alichokuwa akikitamani muda mrefu bali hakuweza kukifanya kwa kutotaka kuzaa nje ya ndoa.

Hakusita kuwaambia madada wa mjini waliokuwa wanamnyemelea kuwa waendelee kushabikia muziki wake lakini habari za mapenzi waziweke pembeni kwa kuwa yeye kwa sasa ni mume wa mama Lolo mtarajiwa hivyo wakae mbali na yeye kwani anaipenda ndoa yake.

 

Chanzo: Enewz

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment