TANZANIA: Bodi ya filamu Tanzania imeikataa script mpya ya video ya Chura ya Snura

 

Mwezi na nusu uliopita, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliifungia video ya wimbo huo na kumwagiza Snura awasilishe script mpya ambayo hata hivyo baada ya kufanya hivyo nayo imekataliwa.

Akiongea na 255 kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM, Snura alidai kuwa baada ya bodi hiyo kukaa kwenye kikao iliona kuwa bado script mpya inataka kufanana na video iliyopigwa marufuku na kumkataza kushoot.

Amedai kuwa jibu hilo lilimchanganya na kumrudisha nyumba na kwamba video ya pili alipanga kuwepo mwenyewe na wala hatocheza zaidi kutembea.

 

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

 

 

Leave your comment