TANZANIA: Malaika na Illuminati?!!!

 

 

Msanii Malaika amezidi kuwaweka watu mbali mbali kwenye kigugumizi juu ya tetesi za yeye ni mshirika wa dini ya kishetani, free mason.

Malaika ambaye wachunguzi wa mambo wamesema anapenda kutumia namba inayohushwa na imani hiyo ya kishetani ya 666, ambayo hata namba yake ya simu inaishia 666, amesema hatolizungumzia suala hilo alipokuwa akiongea na Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema muda muafaka utakapofika ataweka wazi kila kitu.

 

 

 

“Sitopenda kuizungumzia ila niseme tu kwamba ni namba ambayo naipenda, nimepata simu nyingi sana, interviews lakini siku nitakayoamua kuongelea nitaongea kuhusu hivyo, lakini kwa sasa hivi siko tayari”, alisema Malaika.

Pia Malaika amesema hata jina lake la Malaika ambalo watu wanamtuhumu haendani nalo kutokana na mambo hayo, amesema hajali kuhusu hilo kwani hilo ni jina tu kama jina lingine.

Kwenye akaunti yake ya instagram, Malaika ameandika wasifu wenye kushtua watu, ambao amehusisha na Illuminati ndani yake.

 

 

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment