TANZANIA: Wimbo wa Imani ni kwaajili ya kuwapoza wale walioumizwa kimapenzi – Linah
28 June 2016

Linah amesema wimbo wake mpya, Imani ni kwaajili ya kuwapoza wale walioumizwa kimapenzi.
Akiongea na Bongo5 Linah amesema, ” Unajua kila siku tunaimba furaha sana katika mapenzi, je tunawaangalia vipi wale ambao hawana furaha katika mapenzi? Nikaona niimbe wimbo ambao utawatia moyo katika mahusiano yao ambao huwa wanatengwa na familia. Unakuta wanaambiwa kuwa huyo mwanaume maskini, sijui mbaya, unakuta mwingine labda anaambiwa naye mwanamke wako mbaya. Kwa wimbo huu watu kama hao wakiusikiliza wanafarijika sana.”
Kuhusu kurudi kwenye muziki wa injili, Linah amesema, “Kwakweli sina uhakika kwa sasa kama Mungu atanibariki nitaweza au la maana ndio nilipoanzia huko kwahiyo sijajua huko mbeleni.”
Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz




Leave your comment