TANZANIA: Unajua mi mtoto wa kishua - TID

 

 

Msanii TID ameamua kuwajulisha watu siri ya maisha yake, hususan wale wanaomchukulia poa kuwa amechoka, lakini si kweli.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio TID maesema tangu utotoni mwake amelelewa kwenye familia yenye uwezo kipesa, na kumpa urahisi wa kupata akiyoyahitaji kama mtoto.

Akielezea historia ya wimbo wake wa zeze ambao ndio ulimpa umaarufu mkubwa Tanzania na Afrika Mashariki kiujumla, TID amesema yeye ni mtoto wa mjini tena kutoka familia bora.

"Miaka ya 93, 94 kabla baba hajafariki, yeye alikuwa ananipeleka shule town, mimi nimesoma mjini unajua mi mtoto wa kishua, dingi alikuwa na gari alikuwa ananipeleka shule na gari, sasa kila siku nilikuwa nakuta mishe za watu wanapiga zeze, nikamuuliza baba akaniambia hizi ni nyimbo za Wagogo, sasa na mimi nikapata idea pale kwa nini nisiiongezee kitu hii?", alisema TID

TID aliendelea kusema kuwa baada ya hapo ndio akaenda kwa Majani kutaka kurekodi wimbo wa Zeze, lakini Majani alikuwa akimzungusha kila siku, huku akisingizia Juma Nature anarekodi albam.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

Leave your comment