TANZANIA: Huyo Bill Nas kwangu mimi ni chawa tu - TID

 

 

Msanii TID amefunguka na kuonyesha kukereka na kitendo cha msanii Bill Nas ambaye sasa anatamba na ngoma yake ya 'Chafu pozi' kusema kuwa amehama Label ya 'Ladar Entertainment" ambayo ipo chini ya TID.

TID amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo na kudai kuwa aliposikia Bill Nas anasema ametoka kwenye Label yake alikasirika sana kwani alikuwa anachafua label yake hiyo ambayo haikuwa na mkataba wowote na Bill Nas zaidi ya kumsaidia katika kazi zake.

"Unajua ngoja nikwambie jambo Bill Nas alikuja kwangu kutokana na shida zake mwenyewe, mimi nilimsaidia mambo mengi nilikuwa na nunua nguo zake mimi, nimemsaidia kufanya video zake na wala sikuwa na mkataba na yeye alikuja hapa kutokana na shida zake, hata alivyotangaza kuwa ametoka Ladar Entertainment, usiku alinipigia simu na kuniambia braza mimi nipo Ladar ila nilifanya vile ili kukikisha ngoma yangu mpya 'Chafu pozi' nikamwambia wewe nenda tu" alisema TID.

Mbali na hilo TID amemtambulisha msanii mwingine aitwae Chadogy (Mbwa) chini ya Label hiyo na kusema kuwa huyo ana mkataba naye na kufanya naye kazi kama msanii rasmi wa Ladar Entertainment ambaye ana uwezo zaidi ya Bill Nas

" Huyo Bill Nas kwangu mimi ni chawa tu saizi namtambulisha huyo Chadogy kama msanii rasmi huyu si mrithi wa huyo chawa bali huyu ni msanii mkali na mwenye uwezo wa hali ya juu chini la Ladar" alisema TID

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment