TANZANIA: Khaligraph Jones amepanga kufanya ziara nchini Tanzania

 

 

Rapper wa Kenya, Khaligraph Jones amesema amepanga kufanya ziara nchini Tanzania kwaajili ya kujitangaza na kufanya collabo. Amesema ataitumia nafasi hiyo kurekodi ngoma yake na Young Killer – rapper anayemkubali sana kutoka Bongo.

Akiongea na mtangazaji wa Jembe FM, JJ, rapper huyo amesema tayari wamekuwa wakizungumza na Msodoki kwenye WhatsApp na uwezekano wa kufanyika ngoma hiyo ni mkubwa.

“I think there is a possibility of that a collabo [with Young Killer] might be coming soon cause I am planning to tour Tanzania and I am looking forward to work with the guy cause I believe is one of the best rappers not only Tanzania but East Africa, so definitely I am also hoping for the same hii kazi ifanyike na ikifanyika itakuwa noma sana,” alisema Khaligraph. Khaligraph ni mmoja wa rappers wa Kenya wanaoheshimika zaidi kwa sasa.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment

Other news