TANZANIA: Siwezi nikamuimbia mwanaume - Mwasiti

 

 

Mwasiti amesema katika maisha yake yote, kamwe hatokuja kukaa na kumwandikia wimbo mwanaume. Akiongea na kipindi cha Jam Session cha Metro FM ya Mwanza kinachoendeshwa na Jay Joh kujibu swali la kama wimbo wake mpya ‘Unaniangalia’ amemuimbia mwanaume, Mwasiti alisema haitokuja kutokea.

“Sijamuimba mtu yeyote naomba niklie hiyo issue, hiyo ni sanaa,” amesema. “Sitegemea kumuimba mtu yeyote katika career yangu labda nitamuimbia mwanangu na mama yangu. Siwezi nikamuimbia mwanaume kabisa nikakaa chini nadraft hivi, hapana,” aliongeza.

Miongoni mwa mashairi yaliyozua utata kwenye wimbo huo ni pamoja na: Wala hukunipenda mimi,We ulitamani wa mjini, Wamekupiga chini,Unanifuata mimi wa nini!?

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment