TANZANIA: Juma Nature ametoa maoni yake kuhusiana na matumizi ya madawa ya kulevya

 

Juzi ilikuwa ni siku ngumu, ya kishujaa na ya kukumbukwa kwa rapper Young Dee baada ya kuamua kuusema ukweli kuhusiana na tetesi za matumizi ya madawa ya kulevya.

Alikiri kuyatumia kwa mwaka na nusu na kwamba ameacha huku akiahidi maisha mapya na kupendeza zaidi akiwa tena chini ya uongozi wa label ya MDB.

Rapper Juma Nature ametoa maoni yake pia kuhusiana na matumizi ya madawa hayo.

“Kuna mambo ambayo nikijiuliza jibu sipati hivi ni kweli kuna wasanii wanakula mambo hivi, mbona sisi uhuni tumepitia lakini lakaya hii nimpya,” aliandika kwenye Instagram.

“Punguzeni kuiga wadogo zng jamii inawategemea…maana hatatukisema tuwaombeee kazi bure mtarudia tu! Kwani huyo anayewauzia anawashikia bastora ndg zng? Misijapendezwa namichongo famfa kujiendekeza banaaaaa,” aliongeza.

Matumizi ya madawa ya kulevya kwa wasanii yamekuwa hadithi isiyoisha huku Chidi Benz na Ray C wakiwa wahanga waliotawala zaidi headlines kwa sasa.

 

Chanzo: Bongo5

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment