TANZANIA: Tuna project ambayo tunaifanyiakazi - Max

 

 

 

Rapper Young Dee aka ‘rapa paka’ baada siku ya jana kukiri alikuwa anatumia Madawa na kulevya, anajuka na mpango maalum ambao utaweza kuelimisha vijana kuhusu athari za matumizi ya Madawa ya kulevya.

Akiongea na waandishi wa habari Jumatano hii, Mkurugenzi wa label ya MDB ambayo inamsimamia msanii huyo, Max Rioba, alisema tayari wao kama uongozi unaandaa mpango maalum ambao utampa fursa rapa huyo ya kuwaelimisha vijana kuhusu athari za matumizi ya Madawa ya kulevya.

“Tuna project ambayo tunaifanyiakazi, ambayo ziwezi kuiweka wazi zaidi kwa sababu ni mapema,” alisema Max.

“Nina uhakika utakapofikia wakati wake yeyote yule ambaye anataka kuingia kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya atajiuliza mara mbilimbili, sisi tulimuonyesha Young Dee wasanii ambao wameathirika na Madawa ya kulevya, tukamuuliza unataka kuwa kama fulani? Ungependa kesho tuwe na press conference kwamba umekufa? Kwamba tulikuwa na msanii, kwa hiyo kupitia mtindo kama huu utabadili mawazo ya vijana wengi”

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment