TANZANIA: 80% ya video za muziki Tanzania nashoot mimi - Hascana

 

Mtayarishaji wa video za muziki nchini kutoka Wanene Film, Hanscana amesema tayari ameshafanikiwa kuliteka soko la video za muziki nchini ambapo amedai karibu 80% ya video za muziki Tanzania anashoot yeye.

Muongozaji huyo ambaye pia alikuwa mshindi wa Tuzo za Watu 2015 kwenye kipengele cha muongozaji wa video za muziki anayependwa, ameiambia Bongo5 kuwa hali hiyo inamfanya kuwa busy kwa muda mrefu.

“Kwa sasa nafanya kazi kubwa sana, kwa sababu karibu 80% ya video za Tanzania nashoot mimi, na 20% zinaenda kwa wengine, na 10% South Africa,” alisema Hanscan. “Kwa hiyo nakuwa busy sana, madirector wengine wakikaza zaidi tutasaidiana,”

Video ambazo ameongoza hivi karibini ni ‘Bayoyo’ ya AbduKiba, ‘Arosto’ ya G.Nako & Chin Bees & Nikki wa Pili, ‘Freedom’ ya Sugu, ‘My Life’ ya Dogo Janja, ‘Fundi’ ya Mh. Temba pamoja na nyingine nyingi

 

Chanzo: Bongo5

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment