TANZANIA: Jokate na Avril si type yangu - Linex

 

 

Msanii Linex Mjeda leo alitoa nafasi kwa mashabiki wake kumuuliza maswali na yeye kutoa majibu ya maswali hayo kupitia Account yake ya Twitter, ambapo watu mbalimbali waliweza kumuuliza maswali na yeye kutoa majibu ya maswali hayo.

Moja ya shabiki wake alimuuliza kati ya Jokate Mwegelo na msanii wa Kenya, Avril ni yupi anaweza kumchagua ndipo staa huyo ambaye ametamba na ngoma kibao kali aliposema kuwa hajawahi kuwaza jambo hilo, na sababu ya kutokuwaza jambo hilo ni kutokana na ukweli kwamba warembo hao ni wazuri mno kiasi kwamba anahisi yeye si chaguo sahihi kwa watu hao kuotokana na uzuri wao.

"Sijawahi kuwawazia kabisa labda kwa sababu niwazuri sana that's why naona mimi siyo type yao,' aliandika Linex Mjeda.

Lakini mbali na hilo Linex alisema kuwa yeye anafanya muziki kutokana na hisia hivyo asipokuwa na hisia na muziki hawezi kufanya kazi yoyote ile hata wiki nzima au hata zaidi mpaka pale atakapopata hisia za kufanya kazi.

 

E-NEWZ

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment