TANZANIA: Diamond atishia kolabo yake mpya na Psquare

Msanii Diamond Platnum alimaarufu kama Simba ametangaza hali ya hatari kwa kuachia ngoma yake mpya ambayo amefanya na P Square kutoka nchini Nigeria. Diamond Platnum kupitia ukurasa wake wa Instgram alipos picha akiwa na kundi la P Square pamoja na Diamond Pltanumz akiwa na kundi la P Square pamoja na uongozi wake wakitazama kazi yao kabla ya kutoka uongozi wake, huku wakiangalia kazi hiyo kama kufanya mapitio na kuandika kuwa anasikia harufu ya hit song.


Diamond Platnumz ingawa hajaweka wazi lini kazi hiyo inatoka lakini kuna kila dalili kuwa kazi hiyo inaweza kutoka wiki hii kwani tayari ameshaanza kuwaweka sawa mashabiki wake kukaa tayari na kuwa karibu na mitandao yake kwa ajili ya kazi hiyo.


Kitendo cha Diamond kupost picha hiyo na kuandika maneno hayo kumeibua hisia mbalimbali zenye furaha kwa mashabiki wake ambo wengi wameonyesha kuwa na furaha na wakitabiri kuwa huenda ikawa kazi kubwa kutokana na jinsi wanavyomuamini msanii wao na kusema kuwa hajawahi kuwaangusha.
AY ni msanii wa kwanza kwa Tanzania kuwashirikisha P Square katika wimbo wake wa 'Freeze' ambao ulitoka miaka zaidi ya sita iliyopita.

 

 

Leave your comment