TANZANIA: Nina kazi na Chid Benz , sema naogopa kuitoa - Mwasiti

 

 

Msanii Mwasiti Almas amesema Chid Benz ni msanii anayempenda na kumuheshimu sana, kwani amemsaidia kwa kiasi kikubwa mpaka yeye kufika alipo.

Akiongea kwenye PlanetBongo ya East Africa Radio, Mwasiti amesema anampenda sana msanii huyo, kwani ameshafanya mengi na Chidi Benz hivyo anamjua vilivyo, na kwamba hamna msanii bongo mwenye sauti nzuri na tamu kama yake.

Mwasiti ameendelea kusema kuwa alipoanza kufanya naye akzi alikuwa anamuogopa kwani tayari alikuwa ni msanii mkubwa, na yeye ndio akiwa anaanza muziki.

 

Chihd Benz

 

“Chidi alikuwa msanii mkubwa tayari, mi ndo nilikuwa najaribu kufanya muziki unaokimbia alafu nikasema nampenda Chid ana sauti special hakuna aliyenalo Tanzania mpaka sasa, basi nikamuomba tufanye ngoma ya Hao akakubali, tukafanya na mimi nikaanza kupanda jukwaani kufanya fanya show”, alisema Mwasiti.

Pia Mwasiti amesema licha ya hao kuna kazi nyingine aliyoifanya na Chid kabla hajakutwa na matatizo, lakini anaogopa kuitoa kwa sasa, kwani anahofia kumkuta yaliyomkuta Cyril na Raymond, baada ya kumwambia anatafuta kiki kupitia yeye.

'Actualy kuna kazi tumeifanya na Chid, kali sana ila naogopa kuitoa yasije yakanikuta ya Kamikaze na Raymond, (huku akicheka) ila wakati ukifika nitaiachia, ni ngoma kali sana”, alisema Mwasiti kwenye Planet Bongo.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

Leave your comment