TANZANIA: Hakika mitihani humkomaza mtu – Chid Benz

 

 

Msanii Chid Benz alimaarufu kama Chuma amefunguka na kusema kuwa mitihani aliyopata na aliyopitia kwa kipindi cha nyuma imemkuza na amezidi kumuomba Mungu amsimamie ili asiweze kurudi katika mitihani hiyo.

Chid Benz ambaye kwa sasa amezidi kuimarika kiafya amewapa matumaini mashabiki wa muziki wake na wengi wamempongeza kwa hatua aliyofikia sasa huku wengi wao wakiomba arejee kwenye muziki kama zamani, wengine wakimuomba asirudi nyuma alikotoka.

 

 

 

"Hakika mitihani humkomaza mtu, Mungu nisimamie". aliandika Chid Benz kwenye account yake ya Instgram

Hata hivyo mashabiki walikuwa na mengi ya moyoni juu ya muonekano mpya wa Chid Benz pamoja na kitendo alichofanya Babu Tale kuakikisha msanii huyo anaachana na dawa za kulevya.

"Chid Benz yule uliokumbana naye ni shetani na alikuwa anajua kwamba una jambo zuri ndani yako na yeye akataka kukupoteza, una bahati Mwenyezi Mungu bado anakupenda sana akakutoa kwenye yale mateso. Nakuomba uone yale ni matapishi na kamwe huwezi kuyarudia tena mdomoni, najaribu kuangalia familia yako ilikuwa inaumia kiasi gani juu yako, jiulize ni wangapi bado wapo katika hali uliyotoka na hawajapata mtu wakuwashika mikono siyo kwamba wao ndiyo wamemkosea Mwenyez Mungu na wewe ni bora zaidi hapana, jaribu kutambua upendo wa Mungu kwako usirudi nyuma tena. Heshimu kipaji chako kaka, una sauti ya peke yako, unajua muziki, hujawahi toa ngoma mbaya" Watson Lydia

"Sasa usijerudia upumbavu wa madawa ya kulevya tena, si unaona watu tunavyokukubali ona umefungua account siku moja tuu una zaidi ya 11.4 k followers"- Sheby4life

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment