TANZANIA: Wote Diamond na Alikiba nawapenda - Young Killer

 

Msanii anayetamba na kibao cha “Kumekucha”, Young Killer amesema kuwa anawakubali sana Diamond na Alikiba.

 

 

Katika mahojiano yake na Bongo 5 Young Killer amesema kuwa Diamond Platnumz na Alikiba anawakubali:

“Natamani nimshirikishe Diamond kwasababu ni mtu ambaye amefanya vizuri na anainspire, sisi ni wachanaji lakini pia kwa upande mwingine ametuinspire mavideo makali, kafika mbali.

 Mtu wa pili nadhani ni Alikiba kwasababu pia ni muimbaji ambaye nampenda anaimba vizuri, muziki wake mzuri. Nilishawahi kusema kuwa Tanzania wasanii ambao wamewahi kunifanya nitoe hela yangu kununua album yao ni Alikiba. Ni mtu ambaye nilikuwa na dream naye ya kufanya naye kazi. Diamond na Alikiba wote nawapenda 50/50.”

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment