TANZANIA: Diamond na Alikiba walikutana studio na hadi picha walipiga – Babu Tale

 

Diamond Platnumz na Alikiba ni wasanii wanaobeba hisia kubwa za kiushindani katika muziki, jambo lililopelekea kuleta utata hata kwa mashabiki zao. Meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale amethibitisha kuwa wawili hao hawana tatizo lolote, n ahata picha ipo waliopiga wote.

“Kwanza watu wanatakiwa kufahamu kuwa pale sisi tulialikwa kwa ajili ya futari na tulipofika pale wenyeji wetu walituomba sisi kama celebrity kupiga picha ya pamoja na ndio ile picha ambayo tumepiga mimi Alikiba, Ommy Dimpoz na wengine nataka ifahamike kuwa mimi sina tofauti na Alikiba wala Diamond hana tofauti yeyote ile na Alikiba”, alisema Babu Tale

 

 

“Alafu kingine ambacho watu hawakifahamu ni kuwa mwaka jana Diamond na Alikiba walikutana studio na hadi picha walipiga, video pamojana sauti zao pia zipo na hivi karibuni nitaipost ile picha ili kuwaonyesha watu hakuna tatizo ni biashara tu” aliongeza Babu Tale

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment