TANZANIA: Raymond alishafungasha mizigo na kutaka kurudi kwao Mbeya - Madee

 

 

Akiongea kwenya Planet Bongo ya East Africa Radio, Madee amesema Raymond alishafikia hatua ya kufungasha mizigo yake na kuamua kurudi kwao Mbeya, na ingawa alijitahidi kumtuliza lakini hakufanikiwa akaamua kuondoka.

“Raymond alikata tamaa alikuwa anataka kurudi nyumbani Mbeya, mi nilikuwa nipo Mwanza akanipigia simu akawa anakusanya nguo na ilikuwa tayari ni usiku, kwa hiyo alikuwa ameplan asubuhi aende Mbeya, akanielezea kasubiri sana muda unaenda nyumbani wanataka asome, nikajaribu kutumia busara nikamuelezea hata mi unavyoniona nilipofika nimesubiria, lakini alikuwa kama kashaamua hivi, basi nikampa hela akaenda”.

 

 

Madee aliendelea kusema kuwa baada ya kumaliza kusoma alirudi na kuendelea kubaki naye Tip Top, na ndipo apofikia uamuzi wa kwenda nae kila mahali ili asikate tamaa, na Babu Tale akampeleka Yamoto band mpaka akakutana na Diamond.

“Tale naye akamuona akamchukua kaenda nae yamoto band, amekaa sana yamoto band almost mwaka mmoja, baada ya hapo diamond akamuona akampenda, tukakaa mezani akamchukua”, alisema Madee.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment