TANZANIA: Maunda anajipanga kwa ujio wake mpya karibuni – Banana Zorro

 

Msanii wa muziki wa bongo fleva na mmiliki wa band ya B Band, Banana Zorro amefunguka na kuwatoa wasiwasi watanzania kuhusu mdogo wake ambaye alifanya vizuri kwenye muziki wa bongo fleva na nyimbo kama Mapenzi ya Wawili.

Banana Zorro kupitia kipindi cha Planet Bongo alisema kuwa Maunda Zorro saizi anajipanga vyema ili kurudi kwenye game akiwa na nguvu mpya na uwezo wa hali ya juu

 

Maunda Zorro

 

"Nilipenda sana uongee na yeye mwenyewe, ila si mbaya mdogo wangu Maunda Zorro kwa sasa anajipanga vyema kurudi kwenye muziki akiwa na nguvu mpya na uwezo wa hali juu, hivyo naomba watanzania wajue kuwa anajipanga kwa ujio wake mpya karibuni" alisema Banana Zorro.

 

Moja kati ya wimbo wa Maunda Zorro unaozidi kufanya vizuri, ni 'Mapenzi ya wawili', unaweza kutazama video hii hapa:

 

 

Mbali na hilo Banana Zorro aliwaomba wasanii wa sasa kuwa na nidhamu na heshima katika kazi zao ili waweze kudumu kwenye tasnia hiyo kwa muda mrefu kama yeye na kuwa na uwezo wa kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment