TANZANIA: Nimeona ni bora nijisimamie mwenyewe kwa sasa – Mo Music

 

Baada ya kuachana na menejimenti yake, Mo Music amesema kwa sasa anataka kujisimamia mwenyewe kwanza bila menejimenti.

Hivi karibuni Mo Music alivunja mkataba na menejimenti yake iliyokuwa ikisimamia kazi zake kwa madai kuwa wameenda nje ya mkataba wao huku uongozi huo ukidai kuwa yeye ndiye aliyezingua kwenye mkataba wao.

Akiongea na Bongo5, Mo Music amesema kuwa ‘kwa sasa nataka kujisimamia mwenyewe sitaki menejimenti.’

“Mimi nimeona bora nijisimamie kwa muda kwanza, kwa sababu niweke mambo yangu sawa hata kama nikiamua kuchukua menejimenti nijue ipi inanifaa zaidi sitaki kukurupuka. Menejimenti nazozihesabu kama kubwa nne zimenifuata lakini kuna nyingine zinataka zianze kuja,” alisema.

Aidha Mo Music ameongeza kuwa atakuwa makini kuangalia menejimenti nzuri yenye uzoefu na muziki ili yasijitokeze kama yaliyotokea kwenye menejimenti yake ya mwanzo.

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment