TANZANIA: ‘Jike la Shupa’ siyo Shilole - Nuh Mziwanda

 

Nyota wa Bongo Flava Nuh Mziwanda amesema kuwa ngoma yake mpya ya JIKE SHUPA hajamuimbia mtu yeyote mahususi kama inavyodaiwa na baadhi ya wapenzi wa muziki wa kizazi kipya nchini.

Nuh amefunguka hayo jana usiku katika kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV alipokuwa akiizindua rasmi video yake hiyo ya JIKE SHUPA ambayo kwa mara ya kwanza imeruka katika kipindi hicho.

Nyota huyo ambaye alikuwa ni mpenzi wa mwanamuziki mwenzake ambaye pia ni muigizaji wa filamu nchini Zuwena Shaaban a.k.a Shilole ameeleza kushangazwa na baadhi ya watu wanaohusisha ngoma hiyo na Shilole, wakidai kuwa ni ujumbe maalum kwa mwanadada huyo.

Akimzungumzia Video Qeen aliyeshiriki katika video hiyo akivaa uhusika wa jike shupa kufanana na Shilole, Nuh amesema yeye hajui wala haoni kama Video Qeen huyo anafanana na Shilole.

“Uamuzi wa kumtumia huyo dada kwenye hiyo video haukuwa wangu, ni ushauri kutoka kwa director wa video, yeye ndiye aliyepanga kila kitu, kuanzia wahusika hadi script, mimi sikuhusika kwahiyo sikuwa na wazo la kumlenga Shilole kama inavyodaiwa”

Video hiyo imetengenezwa na director Msafiri wa Kwetu Studio.

Katika hatua nyingine, Nuh amesema hivi sasa amekwishasahau maisha yake na Shilole, na ana mpenzi mwingine ambaye mambo yakienda vizuri ndiye atakayekuwa mke wake.

Kuhusu kuchora tattoo ya mpenzi wake mpya kama ilivyokuwa kwa Shilole, Nuh amesema hiyo ni tabia yake kwa kuwa ana mapenzi ya kweli na anapenda kuwa halisi.

“Safari hii tattoo ya mpenzi wangu mpya nimeichora sehemu nyeti zaidi, nah ii ni kuonesha jinsi gani niko Real”. Video ya JIKE SHUPA imeanza kupigwa rasmi jana katika kituo nambari moja cha TV, EATV.

 

Unaweza kuitaza video hapa:

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

Leave your comment