TANZANIA: Harufu ya miguu ya MB Dog ilisababisha aondolewe studio kwa Majani – Madee Ali
6 June 2016

Himaker wa wimbo wa ‘Migulu pande’ Madee Ali amesema kuwa harufu ya miguu ya MB Dog ilisababisha waondolewe studio ya Bongo Records ambayo inamilikiwa na P Funk Majani.
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Madee amesema siku hiyo walikwenda studio kumpeleka MB Dog kurekodi, lakini walipofika studio na kuvua viatu, viliharibu hali ya hewa kutokana na harufu kali.

MB Dog
“Tumeenda kwa mara ya kwanza nimempeleka Mb Dog, mi kipindi hiko nishafanya kazi yake Mola kwa hiyo P funk ananielewa vizuri, kufika getini katufumgulia Kajala, sasa kipindi hicho Mb Dog bado yupo rafu sana havai vizuri, tumeingia studio lakini ratiba anaijua Majani kwamba leo hawa machizi wanafanya ngoma, Mb Dog si kavua viatu bwana, ile harufu ambayo ilikuwa inatokea studio, Majani akamind bwana, akawaka utadhani kimetokea sijui kitu gani huwezi amini hatukurekodi siku hiyo, ilibidi Mb Dog atolewe nje tuanze kuoshana oshana miguu, lakini bado mchizi ikawa tayari kashajitoa kwenye mood hatujarekodi”, alisema Madee.
Madee aliendelea kusema kwamba baada ya tukio hilo Majani aliwataka waende siku nyingine, wakiwa wamevaa ndala ili tukio kama hilo lisijitokeze tena, na wakatekeleza ndipo wakarekodi Latifa.
Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz




Leave your comment