TANZANIA: Namkubali Young Killer - Kaligraph

 

Rapper wa Kenya, Kaligraph amemtaja Young Killer kuwa ndiye rapper anayemkubali na angependa kufanya naye kazi.

Khaligraph anayetamba na wimbo wake ‘Mazishi’ alikuwa akiongea na mtangazaji wa Jembe FM ya Mwanza, JJ na kujibu swali lililomtaka amtaje rapper ambaye angependa kumshirikisha.

“Kwanza ni this young kid nimekuwa nikifuatilia story zake anaitwa Young Killer nikajaribu hata kumshtua kwa Instagram but I havent been getting response from the guy, I don’t know why I think he doesn’t see the messages,” alisema Khaligraph.

“But mimi nikichukua time yangu nimcontact mtu yaani sana sana kwa social media, jua nimekubali kazi yake. So Young Killer I like how his new school with flow and everything ako sawa, so looking forward to work with the guy hopefully in the coming future.”

Khaligraph kwa sasa ndiye rapper anayekubalika zaidi Kenya. So Young Killer check hizo DM bro, ni heshima kubwa huyu jamaa kukubali na kutaka kufanya nawe ngoma.

Chanzo: Bongo5

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment