TANZANIA: Wanaoirudisha nyuma hip hop ni wenyewe wasanii – Fid Q
31 May 2016
Msanii Fid Q amekiri wazi kuwa wasanii wa Hip hop nchini ndiyo chanzo cha muziki huo kushindwa kukua kwa kasi na kuweza kutoboa kimataifa kutokana na wasanii wenyewe wa Hip hop kutotaka kuwekeza katika kazi zao.
Fid Q amesema hayo kupitia kipindi cha eNews na kudai kuwa anakubali kuwa wasanii hao wanaandika vizuri sana, wana midundo mizuri lakini kinachowafelisha ni wasanii hao kutotaka kuweka nguvu kubwa kwenye video zao na kufanya video za kawaida kabisa ambazo zinashindwa kwendana na soko la muziki sasa kitaifa na kimataifa.
Mbali na hilo Fid Q amedai kuwa licha ya Rappers hao kutojiongeza lakini ukweli unabaki pale pale kuwa watanzania na mashabiki wanaupenda sana muziki wa Hip hop.
"Shida ya muziki wa Hip hop bongo ililetwa na bajeti kuwa ndogo kwenye video zetu, unakuta msanii ana bonge la dude lakini video yupo maskani anacheza kamari na masela. Kwa hiyo tukashindwa kudeal na biashara inayoendelea sasa hivi, maana biashara saizi imetoka kwenye show bizz imekwenda kwenye 'eye candy' watu wanahitaji wanahitaji kutazama vitu ambavyo vinawavutia kwenye macho yao. Ndiyo maana unakuta watu kama mimi saizi tunakwea pipa tunakwenda Africa Kusini kushoot video tukiwa na warembo wazuri" alisema Fid Q
"Huu ni muziki kwa kuwa nime rappu bado nipo kwenye misingi na ndiyo maana ukiangalia hata vyombo vya habari vya kimataifa utakuta kuna wasanii wawili au watatu wa Bongo ili hali ukija nyumbani kuna wasanii zaidi ya hamsini wa Hip hop. Kitu kingine kitendo cha kushindwa kuwekeza kwenye video zetu ni sawa na kujishusha wenyewe, leo hata ukiandaa tamasha nakwambia watu wengi wanakuja kwenye tamasha hilo wanakuja kusikiliza na kuona wazee wa Hip hop waje kufanya yao na si hawa wasanii wa bongo fleva hivyo kama watawekeza kwenye video itasaidia Bongo hip hop kukuwa zaidi ndani na nje ya nchi" aliongeza Fid Q
Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz
Leave your comment