TANZANIA: Diamond ashinda taji la Lip Sync Africa
27 May 2016

Diamond Platnumz amechukua taji la kipindi cha Lip Sync Africa kinachorushwa na kituo cha MTV SA.
Alikuwa akichuana na mshkaji wake, Theo wa kundi la Mafikizolo. Kwenye kipindi hicho, wasanii wawili hushindana kuziimba nyimbo za wasanii wengine kwa kugandamizia na kupatikana mshindi mmoja.
Baada ya kuchukua ushindi huo na kupewa mkanda wake, Diamond aliandika kwenye Instagram: Ningependa kumshukuru Mwenyezi Mungu na kuwajuza kuwa kijana wenu nimewawakilisha vyema kwenye mashindano ya LIP SYNC BATTLE AFRICA ya @MtvBaseAfrica na kuweza kuibuka kidedea kwenye Mashindano ya Stage hiyo na kunyakua Mkanda.”
Naye Theo alikubali kushindwa na kumpongeza Diamond kwa ushindi huo.
Lip Sync Battle ni show iliyoanzia Marekani na kuongozwa na rapper LL Cool J na mke wa John Legend, Chrissy Teigen. Kwa Afrika show hiyo inaongozwa na mrembo wa Afrika Kusini Pearl Thusi na staa wa Nigeria, D’Banj




Chanzo: Bongo5
Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz




Leave your comment