TANZANIA: Alikiba aomba watanzania wampigie kura Diamond.
24 May 2016

Msanii wa muziki wa bongo fleva Ali Kiba ameomba watanzania waweze kumpigia kura Diamond katika tuzo za BET zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni huku kwa mara ya pili mfululizo star wa Bongo Flava huyo, ametajwa kuwania tuzo za kimataifa za BET kwenye kipengele cha Best African Act.
Alikiba alisema haya kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kumuombea msanii Diamond Platnum kwa watanzania ili wampigie kura kwenye tuzo anazoshiriki sasa na kusema kuwa yeye ndiye msanii pekee anayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo hivyo watanzania wampigie kura ili aweze kushinda.
Tuzo hizo zitatolewa mwishoni mwa mwezi June nchini Marekani. Diamond pia atatumbuiza June 26 kwenye tuzo hizo.
Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz




Leave your comment