TANZANIA: Diamond atajwa tena kuwania tuzo BET
20 May 2016

Diamond Platnumz ametajwa kwa mara ya pili kuwania tuzo za BET katika kipengele cha Best International Act: Africa. Staa huyo atachuana na nguli wengine wa Afrika wakiwemo Wizkid, Yemi Alade wa Nigeria, AKA, Cassper Nyovest na Black Koffie wa Afrika Kusini na wengine wawili.
Tuzo hizo zitatolewa mwishoni mwa mwezi June nchini Marekani. Diamond pia atatumbuiza June 26 kwenye tuzo hizo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond aliandika na kusema kuwa:
Jus wanted to thank you for your Major Support and let you know that have been nominated for #BETAwards as the Best international Act Africa.... Ningependa niwashukuru kwa Sapoti kubwa Manayozidi kunipa na niwajuze kuwa kijana wenu nimechaguli kuwania tunzo ya Msanii Bora wa Kimataifa toka Africa kwenye tunzo za BET #BETAwards America @BET_Africa @BET_intl
Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz




Leave your comment