TANZANIA: Shilole atangaza vita na msanii mwenzake Vanessa

 

Msanii Shilole ametangaza vita na msanii mwenzake Vanessa mdee, na kusema kuwa asiombe kukutana naye popote.

Akiongea na East Africa TV baada ya kupigiwa smu kujibu tuhuma hizo, Shilole amesema amechukizwa na kitendo cha Vanessa kuandika mambo mabaya juu yake na kupost istagram, hivyo ajiandae kwa lolote.

“Ukiona hivyo ujue kimenuka, kaniongelea shit mi sijapenda, tena mwambieni nikikutana naye atanyooka”, alisema Shilole na kukata simu.

East Africa Tv ilipomtafuta Vanessa Mdee alikataa kuzungumzia suala hilo, ambalo kwa sasa linazidi kukua kwenye mitandao ya kijamii.

Hapo awali ilisambaa post kweny instagram iliypostiwa na Vanessa Mdee akimshambulia Shilole, na ndipo Shilole akapost na video kabisa akisema asioombe akutane naye kwani vibao vyake havielezeki.

 

 

 

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

Leave your comment