TANZANIA: Mwana Fa ampa pongezi AliKiba kwa wimbo "Aje"

 

Msanii wa muziki wa bongo fleva Mwanafalsafa A.K.A Mwana FA amefunguka na kuonyesha hisia zake kuikubali kazi mpya ya msanii Alikiba ambayo inafahamika kwa jina la 'Aje'

Mwana FA kupitia account yake ya twitter aliandika ujumbe wenye kuonyesha kuwa kazi hiyo ya msanii huyo ni kiboko na kusema amesikiliza mara nyingi sana lakini hajaweza kugundua kosa lolote lile kutokana na ngoma hiyo kuwa ni kali.

"hii aje ya kiba nyo*** bana, its perfect Wakazi. Ukiisikiliza mara nyingi kama mimi unakuwa na uwezo wa kuona makosa, Siyaoni hata kwa kuyasaka" Mwana FA

Mbali na Mwana FA msanii mwingine Wakazi pamoja na Shaa wameungana na Mwana FA na kusema kuwa wimbo huo ni kiboko na jinsi ulivyopangiliwa

 

 

 

Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz

 

 

 

 

Leave your comment