TANZANIA: Harmonize na Jackline Wolper mapenzi hadharani…
16 May 2016

Wanasema sharing is caring. Ndiyo maana Harmonize haoni hatari kuweka kambi kwenye koloni la zamani la bosi wake, Diamond.
Inaonekana si tetesi tena kwasababu CEO wa WCB mwenyewe ametoa baraka zake kwa wawili hao, Harmonize na Jacqueline Wolper ambao yeye anawaita ‘love birds.’ Diamond na Wolper waliwahi kuwa na uhusiano miaka kadhaa iliyopita.
Muimbaji huyo wa ‘Make Me Sing’ amepost video inayomuonesha Harmonize akiwa kwenye gari na mpenzi wake huyo mpya huku akimuimbia hit ya bosi wake, Number One.

Unaweza kutazama video yao hapa:
Pakua app ya Mdundo sasa: smarturl.it/mdundo_ig_play_tz




Leave your comment